• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa sera nafuu na fedha kusaidia kupambana na virusi vipya vya korona

    (GMT+08:00) 2020-02-03 17:39:57

    Idara mbalimbali za serikali kuu ya China zimetoa sera nafuu ama fedha ili kuzisaidia serikali za mitaa na watu binafsi katika mapambano dhidi ya virusi vipya vya korona.

    Naibu mkurugenzi wa Kamati ya Afya ya Taifa ya China Bw. Li Bin leo amesema, wagonjwa waliothibitishwa kuambukizwa virusi hivyo watapata ruzuku kutoka kwa serikali kuu na serikali za mitaa kwa ajili ya kugharamia matibabu yao ambayo hayakujumuishwa kwenye bima au msaada wa kimatibabu.

    Wafanyakazi wa matibabu na wengine wanaojihusisha kwenye kazi za kuzuia na kudhibiti virusi hivyo pia watapewa ruzuku, na wale walioambukizwa virusi hivyo wakiwa kazini watalipwa fidia.

    Serikali kuu ya China pia itatoa msaada unaohitajika kwa serikali za mitaa kugharamia vifaa vya matibabu na vipimo ili kupambana na virusi hivyo.

    Wizara ya Fedha ya China imetenga fedha maalum dola za kimarekani milioni 769.8 kuunga mkono serikali za mitaa kote nchini kuzuia na kudhibiti maambukizi ya virusi, ikiwemo dola milioni 215 kwa mkoa wa Hubei, ambao uko mstari wa mbele katika mapambano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako