• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Afrika Kusini aahidi kuboresha uwezeshaji wa kiuchumi kwa wanawake barani Afrika

    (GMT+08:00) 2020-02-03 19:35:27

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ameahidi kutumia nafasi ya uenyekiti wa Afrika Kusini katika Umoja wa Afrika (AU) kuboresha uwezeshaji wa kiuchumi kwa wanawake barani Afrika.

    Mwishoni mwa wiki hii, rais Ramaphosa atakwenda Addis Ababa, Ethiopia, kwa ajili ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika ambapo Afrika Kusini itachukua uenyekiti wa Umoja huo kwa mwaka ujao.

    Amesema wakati Eneo la Biashara Huria la Afrika linatarajiwa kuanza kufanya kazi mwaka huu, Afrika ina fursa ya kuhakikisha kuwa wanawake na biashara zinazomilikiwa na wanawake zinafaidika kihalisi kutokana na soko kubwa zaidi duniani la bidhaa na huduma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako