• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Usalama wa boreshwa , na shughuli za uvuvi za anza tena Mto Nile

    (GMT+08:00) 2020-02-03 20:15:27
    Mamlaka na wakaazi Sudan Kusini na Jonglei wanasema, usalama umeimarika kando ya Mto Nile, shughuli za uvuvi zimeanza tena na wenyeji wanatumia tena mto wa Nile kama njia ya kawaida ya usafirishaji.

    Miezi miwili iliyopita, watu kadhaa waliuawa kwenye kisiwa cha Cuet-Akwet baada ya kutokea mapigano kati ya jamii za wapinzani.

    Wavuvi wanasema kuna maeneo ambayo hawakuweza kufika kwa sababu ya usalama wao, lakini Katika siku chache zilizopita, wameweza kuvua samaki katika maeneo hayo baada ya usalama kuimarishwa.

    Amani inadumishwa katika eneo hilo la mto Nile hadi pale suluhisho la utawala litakapopatikana kwa mabishano ya jamii hizi ambazo zimekuwa zikipigana juu yake nani anamiliki sehemu gani ya kisiwa hicho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako