• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mahakama ya katiba ya Malawi yabatilisha matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwezi Mei

    (GMT+08:00) 2020-02-04 08:43:43

    Mahakama ya katiba ya Malawi imetangaza kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa Rais uliofanyika mwezi Mei, yaliyompatia ushindi rais wa sasa wa nchi hiyo Peter Mutharika.

    Mahakama hiyo imesema tume ya uchaguzi ya Malawi ilikiuka kanuni kadhaa za sheria ya uchaguzi wa rais na bunge na katiba ya Malawi.

    Mkuu wa jopo la majaji wa mahakama hiyo jaji Healy Potani, amesema kulikuwa na ukiukaji mkubwa wa taratibu, na kufanya matokeo ya uchaguzi kutoaminika.

    Mahakama hiyo imeagiza kuwa uchaguzi mkuu mpya unatakiwa kufanyika ndani ya siku 150 zijazo. Hata hivyo Mahakama hiyo imesema Rais Mutharika na aliyekuwa Makamu wake Bw Salous Chilima wataendelea kuwa kwenye nyadhifa walizokuwa nazo kabla ya Mei mwaka jana, hadi uchaguzi mpya utakapofanyika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako