• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi wa Kenya waanza kuchunguza tukio la kukanyagana liliosababisha vifo 14 vya wanafunzi

    (GMT+08:00) 2020-02-04 09:06:18

    Polisi wa Kenya wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio la kukanyagana lililotokea kwenye shule ya msingi magharibi mwa Kenya ambalo lilisababisha vifo vya wanafunzi 14 na wengine 38 kujeruhiwa.

    Kamamda wa polisi David Kabena amesema tukio hili lilitokea kwenye shule ya msingi ya Kakamega saa 11 jioni, ambapo wanafunzi wengi walikimbia nje ya madarasa.

    Bw. Kabena amesema tukio hilo lilitokea wakati wanafunzi wa darasa la 5 lililoko kwenye ghorofa ya 3 ya jengo la shule walipoondoka. Wanafunzi 13 ambao wengi walianguka kwenye ngazi na kufariki papo hapo, na wengine 39 walipelekwa hospitali, mmoja akafariki baadaye, na wengine wanne walijeruhiwa vibaya. Wanafunzi 20 wametoka hospitali baada ya kutibiwa.

    Habari zinasema mwalimu mmoja alipojaribu kumwadhibu mwanafunzi, wanafunzi wengine walikimbia nje na kwenye kukimbia huko baadhi walianguka kwenye ngazi na kukanyagwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako