• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mahakama ya katiba ya Malawi yatengua matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika Mei mwaka jana

    (GMT+08:00) 2020-02-04 17:00:55

    Mahakama ya Katiba ya Malawi imetengua matokeo ya kura za uchaguzi wa rais uliofanyika Mei mwaka jana ambao ulimpatia ushindi rais wa sasa wa nchi hiyo, Peter Mutharika.

    Matokeo yalimpa Muthariki ushindi kwa kupata kura 1, 940,709 dhidi ya mpinzani wake kutoka upinzani, Lazarus Chakwera aliyejipatia kura 1,781,740, na Saulos Chilima kura 1,018,369.

    Chakwera, ambaye ni mwenyekiti wa chama cha Congress nchini Malawi, na Chilima ambaye anaongoza chama cha Umoja wa Harakati za Mageuzi, walipinga matokeo hayo kwa madai ya kutofuatwa kwa kanuni katika kuhesabu kura.

    Mahakama hiyo imeamuru kuwa uchaguzi mpya ufanyike ndani ya siku 150 baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo. Chilima, ambaye alikuwa wa kwanza kufungua kesi akipinga ushindi wa Mutharika, ataendelea kuwa makamu wa rais mpaka uchaguzi mpya utakapofanyika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako