• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa zamani wa Kenya Daniel Arap Moi afariki dunia

    (GMT+08:00) 2020-02-04 18:04:35

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametangaza kuwa, rais wa zamani wa nchi hiyo Daniel Arap Moi amefariki dunia mapema leo katika Hospitali ya Nairobi, akiwa amezungukwa na familia yake.

    Katika taarifa yake aliyotoa mapema leo, rais Kenyatta amesema, Kenya na Afrika kwa ujumla ilibarikiwa kwa huduma za kujitolea kwa Mzee Moi, ambaye alitumia muda wake mwingi kuihudumia Kenya na Afrika katika ngazi mbalimbali. Amesema kiongozi huyo aliongoza Kenya kwa miaka 24 kuanzia mwaka 1978 hadi mwaka 2002 alipostaafu siasa, ameacha kumbukumbu mahiri nyuma yake, akihudumia Kenya kama mwalimu, msomi, mwanasheria, mbunge, waziri, makamu wa rais, na hatimaye kuwa rais.

    Mzee Moi alizaliwa katika kijiji cha Kabarak, kaunti ya Baringo, Rift Valley, na alilelewa na mjomba wake kufuatia kifo cha baba yake wakati akiwa mdogo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako