• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Israel na Sudan zakubaliana kuanzisha mchakato wa kujenga uhusiano wa kawaida

    (GMT+08:00) 2020-02-04 18:57:42

    Waziri mkuu wa Irael Bw. Benjamin Netanyahu ambaye yuko ziarani nchini Uganda, jana alikutana na Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Sudan Bw. Abdel-Fattah al-Burhan huko Entebe, ambapo walikubaliana kuanzisha mchakazo wa kujenga uhusiano wa kawaida kati ya nchi hizo mbili.

    Taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu wa Israel inasema, katika mazungumzo hayo, Bw. Netanyahu alisema anaamini kuwa Sudan inasonga mbele kwa mwelekeo mpya na sahihi. Kwa upande wake, Bw. Burhan alisema Sudan inataka kujenga nchi ya kisasa na kuondoa hali ya kutengwa duniani.

    Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Israel, kutokana na yaliyomo kwenye mazungumzo hayo, ndege za abiria za Israel zitaruhusiwa kuingia anga la Sudan, na hatua hiyo itapunguza muda wa usafiri kati ya Israel na nchi za Amerika ya Kusini na sehemu nyingine.

    Serikali ya mpito ya Sudan bado haijatoa jibu rasmi kwa tukio hilo.

    Mpaka hivi sasa, miongoi mwa nchi za kiarabu, ni Misri na Jordan tu zilizojenga uhusiano wa kibalozi na Israel. Katika miaka ya karibuni, Israel inajitahidi kujenga uhusiano wa kawaida na nchi nyingi zaidi za kiarabu, ikiwemo Sudan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako