• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umaskini wazidi kuilemea Afrika

    (GMT+08:00) 2020-02-04 19:15:40
    Uchumi wa bara la Afrika unazidi kukua lakini hauwafaidi mamilioni ya Waafrika maskini, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imesema.

    Rais wa AfDB Akinwumi Adesina alisema licha ya ripoti kuonyesha kuwa jumla ya Utajiri wa Afrika (GDP) ulikua kwa asilimia 3.4 mwaka jana, hali hiyo haijawasaidia watu wa kawaida.

    Ripoti ya Shirika la Kutafiti Uchumi wa Afrika (AEO) ya mwaka huu ilisema kuwa kwa jumla, Afrika imekua kwa kiwango cha juu, ikilinganishwa na mataifa mengine duniani.

    Lakini licha ya kusema kuwa Afrika inakua, ripoti hiyo ilisema ni mataifa machache tu barani ambayo yaliripoti kupungua kwa idadi ya watu maskini, pamoja na pengo baina ya maskini na matajiri kupungua.

    Mataifa 18 barani yaliripoti kukua kwa uchumi, kulingana na ripoti hiyo ya AEO.

    Kulingana na banki ya AfDB, uwekezaji katika sekta ya elimu, hasa kwa maskini ni mbinu moja itakayosaidia kupunguza umaskini barani Afrika, pamoja na kuziba pengo kati ya matajiri na maskini.

    Inapendekeza uhamasishaji na ufadhili wa elimu katika miradi kama vile kupeana sare za bure na vitabu, pamoja na kuharamisha kazi kwa watoto na kupandisha hadhi ya ualimu.

    Aidha, inazitaka serikali kuwekeza katika mitaala inayofunza mambo yanayohitajika kazini, ili wanaofuzu wasaidike katika sekta za kibinafsi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako