• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wa uchumi wasema sio sekta zote zitaathiriwa vibaya na maambukizi

    (GMT+08:00) 2020-02-04 19:38:31

    Ripoti iliyotolewa na Taasisi ya masuala ya kimataifa ya Shanghai imeonyesha kuwa, maambukizi ya virus vipya vya korona yanaweza kuathiri vibaya sekta za huduma, utengenezaji na biashara, lakini uchumi wa China una nguvu kubwa ya kukabiliana na athari hizo.

    Ripoti hiyo imechunguza kwa kina maendeleo ya juhudi za China kupambana na virusi vipya vya korona, athari zinazoweza kuletwa na maambukizi hayo na mbinu za kukabiliana nazo. Kuhusu uchumi wa China, ripoti hiyo imesema, si sekta zote zinaathariwa vibaya na maambukizi hayo. Kwa muda mfupi, sekta za bishara mtandanoni, michezo ya mtandaoni na kampuni za burudani zinaweza kunufaika na hali ya hivi sasa. Lakini kwa muda mrefu, China ikiwa ni nchi ya pili yenye nguvu kubwa ya kiuchumi, uwezo wake mkubwa katika matumizi, maendeleo ya miji, na teknolojia za 5G na AI hautapotea kutokana na maambukizi hayo.

    Vile vile ripoti hiyo imeipongeza China kwa kuchukua hatua zinazowajibika katika kuzuia virusi hivyo vipya visienee duniani, hatua ambazo zimelinda usalama wa watu wa China na dunia kwa ujumla.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako