• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yaeleza imani na uwezo wa China wa kushinda mlipuko wa virusi vya korona

    (GMT+08:00) 2020-02-04 19:55:41

    Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Asma Mohamed Abdullah amesema China ina uwezo kamili wa kudhibiti maambukizi ya virusi vipya vya korona mapema iwezekanavyo.

    Akizungumza jana kwa njia ya simu na mwenzake wa China Bw. Wang Yi, Bi. Asma, kwa niaba ya serikali na wananchi wa Sudan, ametoa salamu za pole kwa serikali ya China na watu wake kufuatia mlipuko wa nimonia iliyosababishwa na virusi vipya vya korona.

    Kwa upande wake, Bw. Wang amesema wakati mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ulipotokea barani Afrika, China ilikuwa ni nchi ya kwanza iliyopeleka msaada wa dharura wa uokoaji, na nchi ya kwanza kupeleka timu za matibabu kusaidia kupambana na ugonjwa huo, jambo ambalo limekuwa tukio kubwa na muhimu la uhusiano wa kirafiki kati ya China na Afrika. Bw. Wang ameeleza matumaini yake kuwa watu wa nchi zote za Afrika watakuwa pamoja na watu wa China katika mapambano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako