• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FAO: Pembe ya Afrika ni eneo lililoathiriwa zaidi na uvamizi wa nzige wa jangwani

    (GMT+08:00) 2020-02-05 09:07:02

    Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limesema pembe ya Afrika ni eneo lililoathiriwa zaidi na uvamizi wa nzige wa jangwani kati ya maeneo matatu duniani yanayokabiliwa na janga hilo, mengine mawili yakiwa ni Uganda na Sudan Kusini.

    Taarifa iliyotolewa jana na FAO inasema janga la nzige limetoa tishio kubwa kwa usalama wa chakula na maisha ya watu katika pembe ya Afrika, wakati nzige wanaongezeka nchini Ethiopia na Somalia na kuelekea Kusini hadi nchini Kenya.

    Kwa mujibu wa FAO operesheni za angani na ardhini zinaendelea, lakini bado hazitoshi, ambapo katika kipindi cha kuzaliana kwa nzige mwezi Februari idadi yao itaendelea kuongezeka katika nchi hizo tatu.

    Wiki iliyopita FAO ilitahadharisha kuwa uvamizi mkubwa zaidi wa nzige wa jangwani katika miongo kadhaa iliyopita umetishia usalama wa chakula nchini Ethiopia na katika nchi jirani za Afrika Mashariki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako