• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNHCR yatafuta suluhisho la kudumu kwa wasomali waliopoteza makazi

    (GMT+08:00) 2020-02-05 09:15:16

    Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa mataifa UNHCR limesema linafanya kazi kwa karibu na serikali ya Somalia na wadau wengine kutafuta suluhisho la kudumu kwa wasomali waliokimbia makazi yao kutokana na kukosekana kwa usalama na majanga ya asili.

    Mjumbe maalum wa UNHCR katika pembe ya Afrika Bw. Mohamed Affey, na mwakilishi wa UNHCR nchini Somalia Bw Johann Siffointe wametembelea eneo la makazi ya wakimbizi wa ndani la Wabishabele.

    Kwenye ziara hiyo Bw Affey amesema kukimbia makazi kutokana na kukosekana kwa usalama na majanga ya asili, ni jambo lenye utatanishi sana. Kutokana na kuwa watu milioni 2.6 wamekimbia makazi yao, UNHCR inafanya kazi kwa kushirikiana na serikali katika ngazi zote na wadau wengine, kutafuta suluhisho la kudumu.

    Katika miezi mitatu ya mwaka jana watu laki 4.3 waliathiriwa na mafuriko katika nchi nzima, laki 2.3 wakiwa Belet Weyne.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako