• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kaunti za Kenya zasaini makubaliano kupambana na utapiamlo

    (GMT+08:00) 2020-02-05 09:39:19

    Kaunti nne za Kenya zimesaini makubaliano ya misaada na Shirika la lishe la kimataifa (NI) kupambana na msukosuko wa utapiamlo kwa kaya yenye mapato ya chini.

    Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Bw. Joel Spicer amesema, makubaliano hayo yanaitaka kila kaunti na shirika hilo kutoa dola za Marekani laki 6 kwa miaka mitatu mfululizo kuisaidia Kenya kuboresha hali ya utapiamlo.

    Habari zinasema nchini Kenya, wanawake milioni 1.9 wanakumbwa na utapiamlo na watoto karibu laki 8 hawawezi kufikia uzito wa kawaida, na wengine karibu laki 3 wana uzito kipita kiasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako