Shirika la maendeleo la kiserikali la nchi za Afrika Mashariki (IGAD) limetoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha rais wa pili wa Kenya Daniel arap Moi, ambaye aliaga dunia jana asubuhi mjini Nairobi.
Katibu mtendaji wa IGAD Dk. Workneh Gebeyehu ametoa taarifa akikumbusha mchango muhimu wa Bw. Moi katika kuanzishwa kwa IGAD. Taarifa hiyo imesema Mzee Moi atakumbukwa kutokana na juhudi zake katika mambo ya mazingira, amani na usalama barani Afrika, hasa katika kazi ya uongozi juu ya kuirudisha Somalia kwenye jumuiya ya kimataifa na kuisaidia Sudan Kusini kujipatia uhuru.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |