• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yaeleza imani yake kuwa China hakika itashinda virusi vya korona

    (GMT+08:00) 2020-02-05 18:19:15

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Tanzania Profesa Palamagamba Kabudi, kuhusu mapambano dhidi ya virusi vipya vya korona.

    Bw. Wang ameishukuru Tanzania kwa kuipa China pole na kuinga mkono, akiahidi kuwa China itaendelea kutoa taarifa kwa uwazi na kufanya ushirikiano na nchi za Afrika ikiwemo Tanzania katika sekta ya afya.

    Profesa Kabudi amesema, Tanzania ikiwa ni ndugu wa karibu wa China, iko bega kwa bega na China katika muda huu mgumu. Tanzania inaishukuru China kwa kuhakikisha usalama wa raia wake walioko nchini China na kukubaliana na tathmini ya Shirika la Afya Duniani WHO. Pia amesema, hatua zinazochukuliwa na China zimefanikiwa kuzuia kuenea kwa virusi vya korona duniani, na Tanzania ina imani kuwa China itashinda virusi hivyo mapema.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako