• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Brookeside yaongeza bei ya bidhaa zake

    (GMT+08:00) 2020-02-05 19:29:17
    Kampuni ya maziwa ya Brookside yenye matawi yake katika nchi kadha za Afrika mashariki imetangaza kuongeza bei ya bidhaa zake. Wanauchumi wanaona hatua hiyo huenda ikawafanya wakulima wengi kuanza kufurahia kutokana na kuongezeka kwa mapato.Hatua hiyo pia inasemekana italeta ushindani mkubwa sana kwenye sekta hiyo. Mwezi jana, rais Uhuru Kenyatta aliitaka wizara ya fedha kutoa jumla ya shilingi laki 5 kwa kampuni ya maziwa ya KCC kwa ajili ya kununua maziwa kutoka kwa wakulima kwa shilingi 33 kwa lita moja ya maziwa.Tangazo hilo linakuja siku chache tu baada ya kampuni ya Brookside gharama ya uzalishaji wa maziwa kwa shilingi 7 kwa lita. Hivi sasa mkulima yeyote atakuwa akipokea shilingi 35 kwa kila lita moja ya maziwa atakayouzia kampuni ya Brookside. Kwa muda wakulima wamekuwa wakilalamikia malipo kidogo lakini hatua ya sasa huenda ikawafurahisha wakulima wengi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako