• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China atoa salamu za pongezi kwa miaka 20 tangu kuzinduliwa kwa FOCAC

    (GMT+08:00) 2020-02-05 20:11:46

    Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za kupongeza kwa miaka 20 tangu kuzinduliwa kwa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC kwa rais Macky Sall wa Senegal, nchi ambayo ni mwenyekiti mwenza wa FOCAC upande wa Afrika.

    Kwenye salamu zake, rais Xi amesisitiza kuwa China inapenda kutekeleza vizuri wajibu wake ikiwa mwenyekiti mwenza wa FOCAC pamoja na Senegal, kutumia fursa hiyo ya miaka 20 tangu kuzinduliwa kwa FOCAC, na kushirikiana na nchi mbalimbali za Afrika kutekeleza kwa pande zote makubaliano yaliyofikiwa kwenye mkutano wa kilele wa FOCAC uliofanyika Beijing. Pia kuhimiza uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Afrika upate maendeleo zaidi, na kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya pande hizo mbili iliyo na uhusiano wa karibu zaidi.

    Rais Xi amemshukuru rais Sall kwa salamu zake wakati China inapambana na maambukizi ya virusi vipya vya korona, akisisitiza kuwa chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, watu wa China wana imani na uwezo wa kushinda vita hivyo.

    Rais Sall, kwa nyakati tofauti alimtumia rais Xi salamu za sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina na maadhimisho ya miaka 20 ya kuzinduliwa kwa FOCAC, na pia ametoa salamu za pole na uungaji mkono kwa China inayokabiliana na maambukizi ya virusi vya korona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako