• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Naibu waziri mkuu wa China asisitiza udhibiti wa mlipuko wa virusi vya korona kwenye maeneo ya vijijini

    (GMT+08:00) 2020-02-06 09:29:55

    Naibu waziri mkuu wa China Bw. Hu Chunhua ametoa wito wa juhudi kubwa zaidi kufanywa ili kuhakikisha ugavi wa bidhaa za kilimo na kuimarisha udhibiti wa maambukizi ya virusi vya korona kwenye maeneo ya vijijini.

    Bw. Hu ambaye pia ni mkuu wa Kikundi cha uongozi cha Baraza la Serikali kinachoshughulikia upunguzaji wa umaskini na maendeleo, alisema hayo kwenye mkutano uliofanyika Jumatano kwa njia ya video. Amesema juhudi zinatakiwa kufanywa kuimarisha uzalishaji na ugavi wa mboga, nyama, mayai na maziwa, nafaka na bidhaa nyingine za mahitaji ya kila siku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako