• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uzalishaji wa maski waendelea kuongezeka China

    (GMT+08:00) 2020-02-06 09:30:24

    Naibu mkurugenzi wa Kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Hao Fuqing, amesema uzalishaji wa maski nchini China umeendelea kuongezeka, na vifaa vilivyochangiwa na nchi za nje pia vitasafirishwa moja kwa moja kwenda mjini Wuhan.

    Bw. Hao Fuqing amesema hadi kufikia Februari 3, uzalishaji wa maski katika mikoa 22 umefikia milioni 14.8, kati yao laki 1.16 ni ya aina ya N95.

    Baada ya mlipuko wa virusi vya korona kuibuka, serikali za nchi 21, na mashirika ya kimataifa ikiwemo Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa, yamechangia vifaa vinavyohitajika kupambana na virusi hivyo, ikiwemo maski, nguo na miwani ya kujikinga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako