Kenya imetenga dola za kimarekani milioni 40 kwa ajili ya mfuko wa kampuni ndogo na zenye ukubwa wa kati SMEs ili kuhimiza ongezeko la uzalishaji wa kilimo nchini humo.
Katibu mkuu tawala wa wizara ya maendeleo ya viwanda ya Kenya Bw. Lawrence Karanja, amesema mfuko huo utazipatia mikopo kampuni ndogo ambazo haziwezi kupata mikopo kutoka benki za biashara.
Kwenye hafla ya usaini wa nyaraka kati ya wizara hiyo na idara 5 zitakazotoa mikopo, Bw. Karanja amesema serikali inatilia mkazo kustawisha kampuni ndogo na zenye ukubwa wa kati ambazo zinatoa nafasi nyingi zaidi za ajira nchini Kenya.
Serikali pia itatoa mafunzo kwa viongozi wa kampuni ndogo ili kuinua uwezo wao wa usimamizi. Bw. Karanja amesema kampuni zisizopungua 400 zitanufaika. Ingawa Kenya ina benki nyingi, bado ni vigumu kwa kampuni ndogo kupata mikopo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |