• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yazindua waraka muhimu wa sera kuhusu kilimo na kazi za vijijini kwa mwaka 2020

    (GMT+08:00) 2020-02-06 17:06:36

    China imetoa waraka wake Namba 1 kwa mwaka 2020 hapo jana, ukitoa mwongozo kwa ajili ya kilimo na kazi za vijijini kwa mwaka 2020.

    Waraka huo umesema, mwaka huu, China inatarajia kumaliza ujenzi wa jamii ya ustawi katika pande zote, ambao pia ni mwaka wa mwisho kwa nchi hiyo kushinda vita dhidi ya umasikini. Ukiwa ni sera ya kwanza kutangazwa na mamlaka kuu za Chna kwa mwaka huu, waraka huo unachukuliwa kama kiashiria cha vipaumbele vya sera.

    Waraka huo umezungumzia maeneo matano, ambayo ni kushinda vita dhidi ya umasikini, kuboresha miundombinu na huduma za umma katika maeneo ya vijijini, kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa muhimu za kilimo, kurahisisha ongezeko la kipato cha wakulima, kuimarisha uongozi ngazi za kata katika maeneo ya vijijini, na kuboresha maeneo dhaifu vijijini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako