• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kukatisha usafiri wa ndege hakusaidii kupambana na maambukizi ya virusi vya korona

    (GMT+08:00) 2020-02-06 18:07:58

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Hua Chunying leo hapa Beijing alisema kuwa, hatua kali za baadhi ya nchi kufuta safari za ndege kati yao na China hazisaidii kupambana na maambukizi ya virusi vya korona, lakini zimeleta wasiwasi kwa makusudi, kuathiri vibaya mawasiliano na ushirikiano wa kawadia wa kimataifa, na kusumbua utaratibu wa usarifi wa anga wa kimataifa.

    Bi. Hua Chunying amesema kuwa, baada ya kutokea maambukizi ya virusi vipya vya korona, China imechukua hatua kali na za pande zote kupambana na virusi hivyo, na juhudi zake zimeanza kuonesha ufanisi. Shirika la Afya Duniani limezisifu hatua zilizochukuliwa na China, likisisitiza kuwa haliungi mkono kuweka vikwazo vya utalii na biashara dhidi ya China. Kuhusu nchi kadhaa kusitisha usafiri wa ndege, Shirikisho la Safari za Anga la Kimataifa limezihisi nchi hizo kutekeleza pendekezo la WHO. 

    Bi. Hua amezitaka nchi husika zizingatie kwa makini msingi wa kulinda ushirikiano kati ya pande mbili, kurekebisha hatua zao na kuiunga mkono China kwa vitendo halisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako