Marekebisho hayo,ambayo yameongeza haki zote za mizigo kwa mkataba uliopo wa usafiri wa anga,yanatarajiwa kurahisisha usafirishaji wa mizigo.
Marekebisho hayo yameongeza uhuru wa anga kwa shughuli zote za mizigo,ikimaanisha gharama za chini na ufanisi katika usafirishaji mizigo.
Katibu wa serikali ya Amerika anayeshughulika na uchumi na biashara,Manisha Singh na Waziri wa Uchukuzi wa Kenya James Macharia walitia saini mkataba huo alhamisi asubuhi jijini Washington,Marekani.
Waziri Macharia alisema mktaba huo utawezesha upanuzi wa huduma za mizigo za ndege kwa kuruhusu mashirika mengi ya ndege kutoka nchi zote mbili kufungua na kuendesha vituo vya mizigo inayosafirishwa kwa ndege katika nchi zao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |