• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TanTrade imewataka wajasiriamali kuzalisha bidhaa zenye viwango vya kimataifa

    (GMT+08:00) 2020-02-06 19:53:04
    Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imewataka wajasiriamali kuzalisha bidhaa zenye viwango vya ubora wa kimataifa ili zipate soko la uhakika nje ya nchi.

    Akizungumza jana wakati wa mahojiano kwenye maonesho ya wiki ya sheria yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere (Nyerere Square) jijini Dar es salaam jana, Mwanasheria wa Mamlaka hiyo Fikiri Mboya alisema soko la nje lina mahitaji makubwa ya bidhaa kinachotakiwa ni bidhaa kuwa na ubora wa kimataifa.

    Alisema wamekuwa wakiwawezesha wajasiriamali kwa njia ya kuwapa elimu namna ya kuzalisha bidhaa zenye ubora ambazo zinakidhi mahitaji ya ndani na nje nchi. Alisema mamlaka hiyo imekuwa ikitoa huduma mbalimbali, ikiwemo huduma ya taarifa za biashara kwa kukusanya, kuchambua, kuhifadhi na kutoa taarifa za biashara kwa jamii, wafanyabiashara na wadau mbalimbali.

    Pia kuwajengea uwezo kuwaendeleza wazalishaji, wajasiriamali wadogo kwa kutekeleza programu za kuwajengea uwezo kwa kutoa mafunzo, kliniki za biashara na huduma za ushauri kwa jamii ya wafanyabiashara na hasa kipaumbele kikiwekwa kwa wazalishaji wadogo ili waweze kushindana katika masoko ya ndani, kanda na kimataifa. Aidha, alisema wamekuwa wakifanya tafiti za kibiashara, udadisi wa masoko na maendeleo ya masoko ili kutambua changamoto, mahitaji, mienendo ya masoko, fursa na kuongeza thamani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako