• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa nchi za Afrika waanza mkutano wa kawaida wa Umoja wa Afrika

    (GMT+08:00) 2020-02-06 20:27:19

    Mkutano wa kawaida wa 36 wa Baraza la Utendaji la Umoja wa Afrika unaojumuisha mawaziri kutoka nchi 55 wanachama wa Umoja huo umeanza leo mjini Addis Ababa, Ethiopia.

    Mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa kuandaa ajenda na maamuzi pamoja na maazimio ya mkutano mkuu, ikiwa ni pamoja na mapendekezo ya kujadiliwa na wakuu wa nchi wanachama wa Umoja huo uliopangwa kufanyika kuanzia jumapili hadi jumatatu wiki hii.

    Mkutano huo unafanyika chini ya kaulimbiu ya mwaka 2020, "Kunyamazisha Milio ya Risasi: Kujenga Mazingira Mazuri kwa Maendeleo ya Afrika".

    Vurugu ni moja ya changamoto kubwa katika utekelezaji wa Ajenda ya mwaka 2063, na kaulimbiu ya "Kunyamazisha Milio ya Risasi", ililenga kumaliza aina zote za vita, mapigano ya ndani kwa ndani, uhalifu wa kijinsia, vurugu za kutumia mabavu, na kuzuia mauaji ya kimbari katika bara hilo ikifika mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako