• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya China yaagiza kurejesha uzalishaji sambamba na kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona

    (GMT+08:00) 2020-02-06 20:46:01

    Serikali ya China imeagiza shughuli za uzalishaji zirejeshwe kwa taratibu wakati kazi ya kudhibiti maambukizi ya virusi vipya ya korona inaendelea.

    Hayo yamesemwa katika mkutano wa tume ya serikali kuu ya uongozi wa kazi ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vipya vya korona uliofanyika leo hapa Beijing, ulioendeshwa na waziri mkuu wa China, Li Keqiang. Mkutano huo umeagiza kuendelea kuzingatia kazi ya kudhibiti maambukizi mkoani Hubei, hususan mji wa Wuhan ulioathiriwa vibaya zaidi na maambukizi hayo, na pia serikali kuu itaendelea kupeleka madaktari na wauguzi kwenda Wuhan, na kuongeza vitanda kwa ajili ya wagonjwa.

    Kwa mujibu wa taarifa ya mkutano huo, hali katika sehemu nyingine za China imeanza kutulia, na asilimia ya vifo ni ndogo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako