• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika zachukua hatua kuendeleza sekta ya madini

    (GMT+08:00) 2020-02-07 09:30:44

    Wajumbe wanaohudhuria mkutano wa Indaba kuhusu sekta ya madini barani Afrika, wametoa mwito kwa Afrika kuendeleza sekta ya madini.

    Kwenye mkutano huo wa uwekezaji kwenye sekta ya madini, maofisa wa serikali na viongozi kwenye sekta ya madini wametoa mwito wa kuwepo kwa mageuzi, uhakika wa sera na uvumbuzi ili kuvutia uwekezaji kwenye sekta ya madini.

    Nchi mbalimbali zimetumia mkutano huo kutangaza sekta zao za madini kama sehemu nzuri ya uwekezaji.

    Wajumbe kutoka nchi 40 wameonyesha kuendelea kuvutiwa na sekta ya madini ya Afrika Kusini, kuwa nchi hiyo imeweka kitu kinachotajwa na serikali ya Afrika Kusini kuwa ni mazingira ya kanuni na sera wezeshi kwa sekta ya madini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako