• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AU yasema Sudan kuendelea kuwepo kwenye orodha ya Marekani ya "nchi zinazounga mkono ugaidi" kunaathiri kipindi cha mpito

    (GMT+08:00) 2020-02-07 09:31:05

    Umoja wa Afrika umesisitiza kuwa Sudan kuendelea kuwepo kwenye orodha ya Marekani ya nchi zinazounga mkono ugaidi, kunaendelea kuathiri vibaya hali ya kisiasa, kiuchumi na kiusalama ya nchi hiyo.

    Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika limesema hayo kwenye taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mkutano uliofanyika kuhusu hali ya sasa ya Sudan.

    Baraza hilo pia limezihimiza Sudan na Marekani kushughulikia haraka mambo yaliyosababisha nchi hiyo kuwekwa kwenye orodha ya nchi zinazounga mkono ugaidi, na kukaribisha ahadi ya Marekani kuwa juhudi za pande mbili zitaendelea kutatua tatizo hilo.

    Taarifa pia imekaribisha ahadi ya serikali ya Sudan kuwa itatoa fidia kwa wahanga wa mashambulizi ya kigaidi dhidi ya balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998, na dhidi ya manowari ya Marekani ya USS Cole mwaka 2000, ikiwa ni moja ya masharti kwa nchi hiyo kuondolewa kwenye orodha hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako