• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe yaipongeza China kwa juhudi thabiti za kupambana na mlipuko wa virusi vya korona

    (GMT+08:00) 2020-02-07 09:34:03

    Waziri wa afya wa Zimbabwe Bw. Obadiah Moyo ameipingeza China kwa juhudi zake thabiti za kupambana na mlipuko wa virusi vipya vya korona.

    Amesema Zimbabwe ina imani kwamba China itadhibiti virusi hivi, na inaridhika na juhudi zinazofanywa na serikali ya China.

    Amesema China imepata maendeleo yanayostahili kupongezwa katika udhibiti wa virusi hivi, na watafiti wake wamekuwa wanatafiti chanjo ya ugonjwa huo.

    China imeahidi kuisaidia Zimbabwe kuandaa vitengo vya karantini kwa walioambukizwa virusi hivi kwenye hospitali kote nchini humo, na kikundi cha pamoja cha madaktari wa Zimbabwe na China kimeundwa ili kukabiliana na virusi hivi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako