• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AU yataka kutumia AfCFTA kutuliza migogoro barani humo

    (GMT+08:00) 2020-02-07 09:40:26

    Ofisa mwandamizi wa Umoja wa Afrika amesema eneo la biashara huria la Afrika AfCFTA litachangia kutuliza migogoro barani Afrika, kwa kutimiza mchakato wa kuhimiza ustawi wa pamoja barani humo.

    Mkutano wa 33 wa kilele wa Umoja wa Afrika utafanyika Addis Ababa chini ya kauli mbiu ya "Kuacha Mapambano: Kujenga Mazingira Yanayosaidia Maendeleo ya Afrika".

    Kamishna wa Umoja wa Afrika anayeshughulikia biashara na viwanda, Bw. Muchanga Albert amesema AfCFTA ikiwa ni mpango wa maendeleo, limepanua nafasi ya sera kwa maendeleo na kukamilisha mpango wa kutuliza migogoro.

    Amesema, watu wanaounga mkono kuhimiza biashara huria kwa muda mrefu wamesisitiza kuwa manufaa ya biashara huria siyo kwa uchumi tu, bali pia inahimiza watu kuishi kwa amani, na kupunguza uwezekano wa kutokea vita kwa kuzifanya nchi mbalimbali kutegemeana zaidi kiuchumi, kwa sababu biashara huria inatoa faida zaidi kwa watu wa nchi moja kutoa bidhaa na huduma kwa watu wa nchi nyingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako