• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mratibu wa suala la Sudan Kusini apanga kuanza usuluhishi

    (GMT+08:00) 2020-02-07 09:45:21

    Makamu rais wa Afrika Kusini Bw. David Mabuza amesema, amepanga kushauriana na Umoja wa Afrika na nchi husika kutatua suala la idadi ya majimbo linalokwamisha kuundwa kwa serikali ya pamoja ya Sudan Kusini.

    Bw. Mabuza aliyefanya uratibu kati ya serikali ya Sudan Kusini na kundi la upinzani la SPLM-IO, atashirikiana na Umoja wa Afrika na Shirika la IGAD kutafuta njia mwafaka ya kuondoa mgogoro wa kisiasa na mipaka inayokwamisha amani nchini humo.

    Bw. Mabuza pia amesema pande hizo mbili zimeahidi kuunda serikali ya umoja kabla ya tarehe 22 mwezi huu, na kutaka upatanishi ufanyike kabla ya hapo. Hivyo timu yake ya uratibu inahitaji kushauriana na mashirika ya kikanda ili kuongeza ufanisi wa usuluhishi ndani ya muda mfupi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako