• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yakodi ndege ya kunyunyiza dawa dhidi ya nzige wa janwani

    (GMT+08:00) 2020-02-07 09:51:46

    Waziri wa kilimo wa Tanzania Bw. Japhet Hasunga jana akizungumza na wanahabari mjini Dodoma amesema serikali ya Tanzania imekodi ndege ya kunyunyiza dawa kutoka Shirika la kupambana na nzige wa jangwani la Afrika Mashariki, ili kujiandaa kukabiliana na uvamizi wa nzige wa jangwani nchini humo.

    Amesema serikali imechukua hatua zote dhidi ya wadudu hao ambao wameharibu mazao mengi nchini Kenya. Pia ametoa wito kwa wananchi waripoti kwa serikali mara moja dalili za kuwepo kwa wadudu hao. Ameongeza kuwa maeneo ya Katavi na Kigoma yamekumbwa na dalili ya kuwepo kwa nzige wa jangwani.

    Waziri mkuu wa Tanzania Bw. Kassim Majaliwa tarehe 30 mwezi uliopita alisema Tanzania imechukua hatua nyingi kujilinda dhidi ya nzige wa jangwani kutoka nchi jirani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako