• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Formula 1 inafikiria kupanga tarehe nyingine ya mbio za Grand Prix za China

  (GMT+08:00) 2020-02-07 10:12:11

  Formula 1 inafikiria kupanga tarehe nyingine ya mbio za Grand Prix za China kama hazitaweza kufanyika katika tarehe yake ya awali kwasababu ya mlipuko wa virusi vya korona. Mbio hizo zilipangwa kufanyika Aprili 19 lakini hakuna uhakika kutokana na ugonjwa huo. Formula 1 imesema wataacha wazi nafasi kuona kama mbio zinaweza kufanyika baadaye mwaka huu kwani wanapenda mbio zifanyikie China. Hali hiyo imejadiliwa kwenye mkutano wa kundi la mkakati la F1 wakiwepo mabosi na timu juzi Jumatano bila kufikia maamuzi. F1 inasubiri mamlaka za China ili kutoa maamuzi juu ya mbio hizo za langalanga. Lengo la mwanzo lilikuwa ni kufanya mbio hizo baadaye mwaka huu lakini timu zilikataa na mbio kuahirishwa. Mara ya mwisho kuahirishwa kwa mbio za langalanaga ilikuwa mwaka 2011, wakati Bahrain Grand Prix zilipoathirika na harakati za Arab Spring.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako