• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya mambo ya nje ya China yasema urafiki kati ya China na Afrika hauwezi kutikiswa kutokana na uchokozi wa mtu fulani

    (GMT+08:00) 2020-02-08 19:30:59

    Gazeti la Financial Times limesema ofisa wa serikali ya Marekani amesema kuwa serikali hiyo inataka kuizuia China kuzisaidia nchi za Afrika kujenga kituo cha udhibiti na kinga ya maradhi cha Afrika kutokana na kisingizio cha shughuli za ujasusi za sayansi zinazopangwa na China, huku akisema China inataka kuibia takwimu za jeni za Afrika kupitia kujenga kituo hicho.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Hua Chunying amejibu kuwa hoja hiyo haina msingi wowote, na inaonesha baadhi ya watu wa Marekani wanaitazamia China kwa uhasama. Amesema urafiki kati ya China na Afrika hauwezi kutikiswa na uchokozi wa mtu fulani.

    Bi Hua amesema mwaka 2014 mlipuko wa virusi vya Ebola uliotokea Afrika Magharibi umeonesha udhaifu wa mfumo wa afya ya umma wa Afrika, na Afrika inaitaka jumuiya ya kimataifa kuiunga mkono kujenga kituo cha udhibiti na kinga ya maradhi cha Afrika. Mwaka 2015, China ilishiriki kwa udhati kwenye kujenga uwezo na mfumo wa afya ya umma barani Afrika. Mwaka 2016, China na Marekani zilisaini makubaliano ya kuunga mkono ujenzi wa kituo cha udhibiti na kinga ya maradhi cha Afrika, ili kusaidia kuimarisha uwezo wa usalama wa afya ya umma barani humo. Pande zote pia zimetuma wataalamu kuwa washauri na kutoa uungaji mkono wa kiteknolojia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako