• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shambulizi dhidi ya kijiji lasababisha vifo vya raia watano magharibi mwa Niger

    (GMT+08:00) 2020-02-08 19:33:20

    Vyombo vya habari vya Niger vimesema watu wenye silaha wasiojulikana wameshambulia kijiji kilichoko mkoani Tillaberi, magharibi mwa Niger na kusababisha vifo vya raia watano.

    Ripoti zinasema watu wanne wenye silaha juzi asubuhi walivamia kijiji hicho na kushambulia eneo la ujenzi na kusababisha vifo vya wafanyakazi watatu wa ujenzi na mmoja kujeruhiwa vibaya ambaye alifariki baada ya kupelekwa hospitali. Baada ya hapo, watu hao wenye silaha walimshambulia mwalimu aliyekuwa karibu, ambaye alifariki papo hapo.

    Katika miaka ya hivi karibuni, makundi ya kigaidi yamefanya mashambulizi mengi katika maeneo ya mpakani kati ya Niger, Mali na Burkina Faso na kusababisha vifo na majeruhi ya watu wengi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako