• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FAO yasema watu milioni 239 wa Afrika kusini mwa sahara wanataabika na njaa na utapiamlo

    (GMT+08:00) 2020-02-09 17:08:24

    Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Matiafa FAO Marina Helena Semedo amesema watu takriban milioni 239 wa Afrika kusini mwa sahara wanataabika na njaa na utapiamlo, na kusisitiza njia pekee ya kutokomeza kabisa taabu hizo ni kupitia amani na usalama.

    Bi Semedo amebainisha kuwa Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa yameweka shabaha kadha muhimu ikiwemo kupunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya Waafrika walio kusini mwa sahara ambao wanaishi na umasikini, njaa, na utapiamlo, kwa kuwawezesha kwenye kilimo kinachoungwa mkono ili kusukuma mbele juhudi za nchi za kufikia ajenda ya maendeleo endelevu ya 2030.

    Mbali na hayo Bi Semedo pia amesititiza FAO hivi sasa inatekeleza shughuli mbalimbali za kuongeza mapato kwa ajili ya watu wa vijijini walio masikini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako