• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Afrika Kusini achukua uenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika

    (GMT+08:00) 2020-02-10 08:19:20

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amechukua uenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika, kwenye ufunguzi wa mkutano wa 33 wa kilele unaofanyika mjini Addis Ababa. Mkutano huo unafanyika chini ya kauli mbiu ya "kutuliza migogoro: kuweka mazingira mazuri kwa maendeleo ya Afrika".

    Rais Ramaphosa anachukua nafasi hiyo kutoka kwa mwenyekiti aliyemaliza muda wake, ambaye ni Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi. Rais Ramaphosa amesema katika kipindi chake atafanya juhudi kuhimiza vipaumbele vya maendeleo, na kuweka mkazo kwenye ushirikiano kati ya nchi wanachama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako