• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa afya wa Uganda apongeza juhudi za China katika kupambana na virusi vya korona

    (GMT+08:00) 2020-02-10 09:48:14

    Waziri wa afya wa Uganda Bibi Robinah Nabbanja ameipongeza China kwa hatua zake madhubuti za kudhibiti mlipuko wa virusi vya korona.

    Bibi Nabbanja amesema China imetambua njia za matibabu zinazofanya kazi, wagonjwa wamepewa matibabu na baadhi yao wanaopata nafuu wametoka hospitali. Anaamini kuwa China ina uwezo wa kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo.

    Amesema hatua za China za kuwaweka karatini wale wanaodhaniwa kuambukizwa virusi vya korona, zinafanya kazi vizuri katika kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo. Pia ameipongeza China kwa kujenga hospitali mpya yenye vitanda elfu moja mjini Wuhan ndani ya siku kumi kwa ajili ya kuwatibu wagonjwa wa virusi vya korona, kitendo ambacho ni muujiza.

    Ameongeza kuwa serikali ya Uganda haina mpango wa kuwarejesha wananchi wake walioko nchini China kutokana na juhudi thabiti zinazofanywa na China kupambana na virusi hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako