• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mlipuko wa Ebola nchini DRC kutathminiwa upya baada ya maendeleo kupatikana

    (GMT+08:00) 2020-02-12 09:29:02

    Kamati ya kimataifa ya dharura ya kiafya kuhusu ugonjwa wa Ebola itakutana kutathmini kama mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC unaendelea kuwa Dharura ya afya ya umma inayotia wasiwasi jumuiya ya kimataifa.

    Kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika jana Jumanne, mkurugenzi mkuu wa Shirika la afya duniani WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuendelea kutoa msaada kwa juhudi za kukabiliana na mlipuko wa Ebola, bila kujali pendekezo litakalotolewa na Kamati ya kimataifa ya dharura ya kiafya.

    Kwa mujibu wa Bw. Ghebreyesus, katika wiki iliyopita, matukio matatu tu ya maambukizi ya Ebola yaliripotiwa, na hakuna maambukizi mapya katika siku tatu zilizopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako