• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mbuga ya Mikumi Tanzania sasa ina tembo zaidi ya elfu 15

    (GMT+08:00) 2020-02-12 09:34:41

    Matokeo ya sensa ya wanyamapori yaliyotangazwa jana, yameonyesha kuwa mbuga ya Selous – Mikumi kwa sasa ina tembo elfu 15. Sensa hiyo ilifanywa chini ya uongozi wa Taasisi ya utafiti wa wanyamapori (TAWIRI) kwa kushirikiana na Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori (TAWA) na Mamlaka ya mbuga za wanyama Tanzania (TANAPA), kati ya mwezi Oktoba na Novemba mwaka 2018.

    Akiongea baada ya kuitangaza matokeo hayo, Waziri wa maliasili na utalii wa Tanzania Dk. Hamisi Kigwangala, amesema matokeo hayo yanaonyesha kuwa juhudi za serikali ya Tanzania kupambana na ujangili zimefanya kazi, na sasa juhudi zinatakiwa kuendelea ili idadi ya tembo iweze kurudi katika hali ya kawaida.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako