• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • WHO yaipa jina nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya Korona kuwa COVID-19

  (GMT+08:00) 2020-02-12 09:50:06

  Kongamano la utafiti na uvumbuzi duniani kuhusu virusi vipya vya Korona limefanyika jana huko Geneva, ambapo mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Bw. Tedros Ghebreyesus ametangaza kuipa jina nimonia inayosababishwa na virusi hiyo kuwa "COVID-19".

  Amesema ni muhimu kuupa jina ugonjwa huo, kwa sababu inaweza kuepuka kutumia majina yasiyo sahihi na ya fedheha, pia inaweka mfano kwa virusi vingine vya Korona vinavyoweza kutokea katika siku za usoni.

  Bw. Tedros pia amesema chanjo ya kwanza ya virusi hivyo inatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 18, hivyo kwa sasa tunapaswa kutumia hatua zote kupambana na virusi hivyo, na kujiandaa kwa mapambano ya muda mrefu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako