• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mitaa ya makazi yawa ngome za kukinga maambukizi nchini China

  (GMT+08:00) 2020-02-12 21:01:48

  Rais Xi Jinping ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China amesisitiza kuwa, mitaa ya makazi iko mstari wa mbele zaidi katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vipya vya korona (COVID-19), na pia ni mstari wenye ufanisi zaidi wa kuzuia maambukizi kutoka nje na kuenea kwa maambukizi ya ndani.

  Rais Xi ameagiza sehemu zote nchini China zizingatie umuhimu wa mitaa ya makazi, na kuongeza juhudi zaidi za kukinga maambukizi kwenye mitaa hiyo, ili kuifanya iwe ngome imara ya kudhibiti maambukizi.

  Baada ya kutokea kwa mlipuko wa COVID-19, serikali kuu na serikali za mitaani zote zinatilia maanani umuhimu wa mitaa ya makazi, zimetoa elimu ya kukinga maambukizi, kupima joto kwa wakati, kuandikisha watu wanaoingia na kutoka, na kuwahudumia vizuri watu waliotengwa wanaoshukiwa kuambukizwa. Wakati huohuo, China imechukua hatua mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya kimsingi ya maisha ya watu, mfano, wafanyakazi wa mitaa wanawanunuliwa wakazi wenye matatizo mahitaji ya kila siku ya maisha.

  Maambukizi hayo ni kama mtihani mkubwa kwa wafanyakazi wa mitaa ya makazi, na pia ni fursa ya kuimarisha mfumo wa usimamizi wa mitaa hiyo. Mitaa ya makazi katika sehemu mbalimbali nchini China inatakiwa kutekeleza kwa makini maagizo ya serikali kuu, kutegemea na kuhamisisha watu, ili kuanzisha mazingira mazuri kwa ajili ya China kushinda vita dhidi ya maambukizi hayo mapema.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako