• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Simba, Yanga Ubingwa Upo Hapa!

  (GMT+08:00) 2020-02-13 17:06:30

  Hivi sasa Simba inaongoza Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 53, huku Yanga ikiwa ni ya tatu na pointi zake 38. Simba ikiwa imecheza mechi 21 na Yanga 19, zinatarajiwa kupambana Machi 8, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, mchezo unaotajwa kuwa ndiyo utaamua bingwa wa ligi msimu huu. Kama ilivyokuwa katika mchezo wa mzunguko wa kwanza baina ya timu hizo, ndiyo ilivyo mchezo huu kwani awali ilionekana atakayeshinda ndiye ana nafasi kubwa ya kuwa bingwa, lakini mwisho wa siku matokeo yakawa 2-2. Kuelekea mchezo huu wa mzunguko wa pili, Yanga inatarajiwa kucheza mechi tano kabla ya kukutana na Simba. Safari hii Yanga watakuwa wenyeji wa mchezo huo. Kwa upande wa Simba, nao watacheza mechi tano kabla ya kukutana na Yanga. Mechi hizo zinatajwa kuwa zinaweza kuwa kikwazo kwa wote katika kuelekea kutwaa ubingwa msimu huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako