• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kujitahidi kutimiza malengo ya maendeleo kwa mwaka huu

  (GMT+08:00) 2020-02-13 19:23:09

  Maambukizi ya COVID-19 yaliyotokea ghafla ni changamoto kubwa inayokabili China, na pia yameleta wasiwasi kwa dunia nzima.

  Mkutano wa wajumbe wa kudumu wa ofisi ya siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China uliofanyika jana mjini Beijing umesema, maambukizi hayo yamekuwa na mabadiliko mazuri, na kazi za kupambana na maambukizi hayo zimepata ufanisi.Mkutano huo pia umesema China itahimiza maendeleo ya uchumi na jamii wakati inapopambana na maambukizi, na athari ya maambukizi kwa uchumi na jamii inatokana na ufanisi wa juhudi zilizochukuliwa. Hivi sasa ufanisi huo umepatikana, na kuweka msingi mzuri kwa ajili ya kutimiza malengo ya maendeleo ya mwaka huu.

  Mkutano huo pia umepangilia hatua za kudumisha utulivu wa maendeleo ya uchumi na namna ya kuvisaidia viwanda kurejesha uzalishaji. Hatua hizo ni pamoja na sera ya fedha, kupunguza kodi, sera nafuu ya mikopo, na sera ya kuhimiza ajira. Mwaka huu, China itakamilisha ujenzi wa jamii yenye maisha bora. Japo inakabiliwa na maambukizi, Wachina watajitahidi kutimiza malengo yaliyowekwa ya maendeleo. Ili kutumiza malengo hayo, jambo muhimu zaidi ni mshikamano.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako