• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kituo cha mpakani cha Nimule kupiga jeki ushirikiano wa biashara kati ya Uganda na Sudan kusini

  (GMT+08:00) 2020-02-13 19:39:35

  Uganda inatarajia kuongeza kiwango cha baishara katia yake na Sudan Kusini kufutaia kukamilika na kukabidhiwa kwa awamu ya kwanza ya Kituo kimoja cha mpaka (OSBP) kwa serikali ya Juba.

  Kituo cha mpaka cha Nimule kitasimamiwa na maafisa wa forodha kutoka Sudan kusini ,na iwapo kitafanya kazi inavyopaswa,hakuna sababu kwa nini biashara ya kikanda isiimarike.

  Akizungumza baada ya kukabidhiwa rasmi kwa kituo cha Nimule,Waziri wa Biashara,Viwanda na Vyama vya Ushirika wa Uganda Bi Amelia Anne Kyambadde alikitaja kituo hicho kilichogharimu $5million (takriban UShs 18.3billion) ,ufadhili kutoka serikali ya Uingereza kupitia shirika la TradeMark East Africa (TMEA) kama maendeleo mazuri sio tu kwa Sudan Kusini naUganda lakini kwa ukanda mzima wa Afrika Mashariki.

  Alisema kufunguliwa kwa kituo cha mpakani cha Nimule ,anatarajia kuongezeka kwa biashara.

  Alisema Uganda inatarajia kuongeza biashara na Sudan Kusini kwa $500million kufikia mwisho wa mwaka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako