• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wataalamu wahimiza kuimarisha mafungamano ya kiuchumi barani Afrika kwa kupitia uanachama wa WTO na utekelezaji wa AfCFTA

  (GMT+08:00) 2020-02-14 10:24:11

  Wachumi na watunga sera wa Afrika walioshiriki kwenye mazungumzo ya kikanda ya Shirika la biashara duniani (WTO), wamesisitiza mahitaji ya haraka ya kuimarisha mafungamano ya kiuchumi barani Afrika kupitia uanachama wa WTO na utekelezaji wenye ufanisi wa Makubaliano ya biashara huria ya bara la Afrika (AfCFTA).

  Mwito huo umetolewa kwenye mazungumzo ya tatu kuhusu kujiunga na WTO kwa Afrika, ambayo yalifanyika huko Addis Ababa kuanzia tarehe 12 hadi 14.

  Kamishna wa Umoja wa Afrika anayeshughulikia mambo ya biashara na viwanda Bw. Albert Muchanga, amesema Afrika inafanya juhudi kuunga mkono mfumo wa pande nyingi, wakati vitendo vya kujilinda kibiashara vikiongezeka duniani.

  Amesema Afrika inatoa mchango kwa mfumo wa pande nyingi kutokana na kuwa nchi za Afrika zinajiunga na WTO, na makubaliano ya AfCFTA yanakamilishwa wakati hatua za kujilinda kibiashara zinapoongezeka duniani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako