• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marekani yatarajia kufikia makubaliano na kundi la Taliban nchini Afghanistan

  (GMT+08:00) 2020-02-14 19:01:38

  Rais Donald Trump wa Marekani jana amesema nchi hiyo inatarajia kufikia makubaliano na kundi la Taliban ndani ya mwezi huu juu ya kuondoa jeshi la Marekani nchini Afghanistan.

  Kauli hiyo ya Trump inaonyesha maendeleo makubwa yaliyopatikana tangu Marekani na kundi la Taliban zilipofanya mazungumzo mwezi Desemba mwaka jana nchini Qatar. Awali, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo alisema mazungumzo hayo yamepata maendeleo muhimu sana. Waziri wa ulinzi wa Marekani Bw. Mark Esper amesema pande mbili zinafanya mazungumzo juu ya suala la kupunguza mapambano kwa siku saba, ambalo linatazamiwa kuwa ni changamoto kwa viongozi wa kundi la Taliban katika kudhibiti wapiganaji wake.

  Habari zinasema Marekani na kundi la Taliban zinatarajiwa kusaini makubaliano ya amani mwezi huu, kitendo ambacho kitawafanya askari elfu 13 wa Marekani na maelfu ya watu wa NATO waondoe kutoka Afghanistan.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako