• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yapenda kushirikiana na Marekani katika kukabiliana na COVID-19

  (GMT+08:00) 2020-02-14 19:06:32

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Geng Shuang amesema, tangu mlipuko wa maambukizi ya virusi vipya vya Korona COVID-19 utokee, China imedumisha msimamo chanya na wazi kuhusu ushirikiano na Marekani, na itaendelea kushirikiana na jamii ya kimataifa ikiwemo Marekani kukabiliana na maambukizi, ili kulinda usalama wa afya duniani.

  Mkurugenzi wa Kamati ya Uchumi ya Ikulu ya Marekani Larry Kudlow amesema, anasikitika kuwa, China haijaialika Marekani kushiriki kwenye juhudi za kukabiliana na maambukizi ya korona, na haiko wazi katika maambukizi hayo. Geng amesema, idara za afya za China na Marekani zimedumisha mawasiliano kwa karibu, na wanasayansi wa nchi hizo pia wamefanya mawasiliano ya kiteknolojia kwa njia tofauti. Pia hatua za China za kukabiliana na maambukizi zimepongezwa na rais Donald Trump wa Marekani na waziri wa afya wa nchi hiyo Alex Azar.

  Wakati huohuo, mkutano wa dharura wa mawaziri wa afya wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya umetangaza kuwa, hakuna haja ya kupiga marufuku watalii wa China kuingia kwenye eneo la Schengen. Geng amesema China inakaribisha uamuzi huo, na kuushukuru Umoja huo kwa kuunga mkono mapambano dhidi ya maambukizi ya korona.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako