• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Joshua Cheptegei avunja rikodi ya Kipruto ya km 5

    (GMT+08:00) 2020-02-17 10:41:51

    Mwanariadha wa Uganda Joshua Cheptegei jana aliweka rikodi ya dunia kwa mbio za km 5 akitumia muda wa dakika 12 na sekunde 51. Bingwa huyo wa dunia wa mita 10,000 ametumia vizuri mazingira katika makala ya pili ya mbio hizi kuvunja rikodi iliyowekwa na Mkenya Rhonex Kipruto ya dakika 13 na sekunde 18 mwezi uliopita huko Valencia. Oktoba mwaka jana Cheptegei alichukua medali ya dhahabu kwenye mbio za mita 10,000 za mabingwa wa dunia zilizofanyika Doha, huku Kipruto akiweka kibindoni medali ya shaba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako